Chile imefanikiwa kuing’oa Ureno katika michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini Urusi kwa kuitandika penati 3-0.

Aidha, katika mchezo huo mlinda mlango wa timu ya taifa ya Chile, Claudio Bravo ameibuka kuwa mchezaji bora katika mchezo huo mara baada ya kuokoa mikwaju ya penati tatu dhidi ya Ureno.

Bravo alifanikiwa kuokoa mikwaju hiyo ya penati zilizopigwa na Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Nani huku Chile wakifanikiwa kupata penalti tatu.

Hata hivyo, Chile itamenyana na kati ya timu mbili ya Ujerumani ama Mexico zinazotarajiwa kuumana mapema hii leo ili kuweza kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe hilo la mabara itakayochezwa siku ya jumapili.

 

?LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 29, 2017
Video: Giza nene mauaji Kibiti, DPP sasa asubiri faili la Lowassa