Mwimbaji mweye uwezo wa ku-switch mitindo zaidi ya mitatu, Chin Bees amefunguka kuhusu wimbo wake mpya alioubatiza jina la ‘Nyonga-Nyonga’, alioufanya chini ya Wanene Entertainment.

Chin Bees ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano ndani ya ‘Burudani 24’ ya Dar 24 ameanika kilichojili wakati wa utayarishaji wa wimbo huo na jinsi alivyowahi kuwashangaza watayarishaji ndani ya studio za Wanene Entertainment waliomtupia mfupa wa mdundo kisha akaurarua.

Katika hatua nyingine, msanii huyo aliyewahi kunogesha vibwagizo vya hits kadhaa ikiwa ni pamoja na ‘Arosto’ya G-Nako na ‘Sweet Mangi’ ya Nikki wa Pili, ameanika chanzo cha ugomvi kati yake na kundi la Navy Kenzo.

Mkali huyo wa ‘Nyonga-Nyonga ameeleza pia jinsi alivyokuwa akishiriki katika uandishi wa baadhi ya nyimbo za Navy Kenzo ikiwa ni pamoja na hit ya ‘Game’, alieleza pia kinachoweza kufanyika ili alewane na kundi hilo.

Mbali na hayo yote, Chin Bees ameeleza kitakachojili hivi karibuni kwenye maisha yake ya muziki na jinsi alivyoji-set kulipuka mfululizo na ngoma zitakazoacha alama kubwa.

Mbunge wa Mikumi, Joseph ‘Profesa Jay’ Haule, na rapa Jay Mo walikuwa sehemu ya maelezo ya Cheen Bees. Usikubali kupitwa na mahojiano haya, enjoy:

Cristiano Ronaldo kutupwa jela kwa kukwepa kodi
P Diddy awaburuza mastaa, atajwa Forbes

Comments

comments