Mkuu wa Wilaya Dodoma mjini, Patrobas Katambi amemtaka Msanii wa vichekesho nchini, Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la Masanja mkandamizaji kuripoti Kituo cha Polisi ndani ya siku tatu baada ya kuonyesha mzaha katika ugonjwa wa virusi vya Corona.

Katambi amesema kuwa dunia nzima inahaha kutafuta suluhu chakushangaza Masanja anafanya mzaha hivyo atatakiwa kwenda Polisi kueleza alikuwa anamaanisha kitu gani.

Kupitia mtandao wa kijamii wa DW swahili  pamoja na Masanja alichapisha video katika mitandao ya kijamii akifanya mzaha kwa kuhoji watu kuhusiana na ugonjwa wa Corona ambapo baadhi ya watu aliokuwa akiwahoji, walisema wanahitaji covid-19 wapatiwe nyingi.

Hata hivyo Katambi amesema Rais John Magufuli alichukulia uzito mkubwa wa tatizo hilo hapa nchini na kutoa tahadhari kwa Wananchi “sasa huyu Masanja yeye ni nani inamaana anapingana na Rais”.

Aidha amesema Masanja alifanya tukio hilo akitumia neno la kiingereza la Covid-19, ambapo alitaka kuonyesha Wananchi wa Dodoma hawana uelewa wa ugonjwa huo.

EPL yapigwa tena kalenda
Corona Kenya: Mtoto wa miaka 6 afariki, wagonjwa wafika 122

Comments

comments