Rapa kutoka Mwanza, Coyo ambaye hivi karibuni alitikisa na ‘Ziwafikie’, ameshindilia msumari mwingine mkubwa zaidi kupitia video ya wimbo wake mpya ‘Itakucost’.

Katika video hiyo mpya iliyoongozwa na Destro wa kampuni ya kimataifa ya Wanene Entertainment, mchekeshaji anayeishika mitandao ya kijamii kwa vituko vyake akifahamika kwa jina la ‘Mkali Wenu’ atakuvunja mbavu na jinsi anavyorukia yasiyo ya kiwango chake, kweli ‘Inamcost’.

Ubora wa video hii utakupa tafsiri halisi ya kwanini wasanii wa Tanzania hawapaswi kupoteza nauli kwenda ughaibuni kutafuta eneo zuri la kufanya video au waongozaji wengine.

“Video imefanyika hapahapa Tanzania tena ndani ya studio za Wanene Entertainment. Audio imetayarishwa na mimi na Daydream wa studio za Over The Classic zilizoko Mwanza,” Kidbwoy ambaye ni meneja wa Tetemesha Records  inayosimamia muziki wa Coyo imeidokeza Dar24.

Ubora huo umeeendelea kwenye audio ya wimbo, mashairi na ‘of course’ warembo na watanashati walioing’arisha zaidi. Ukiimaliza kuangalia video hii huenda ukampandisha daraja moja rapa huyu kutoka Mwanza ambaye kila wimbo wake huwa na maneno ya lugha ya ‘Kisukuma’.

Endelea kutembelea Dar24, tutamvuta hapa afunguke yote yanayoihusu ‘Itakucost’.

Simon Msuva kuchezea soka Morocco
Saida Karoli: Jina liliniletea dhihaka, dharau za wazi na kutukanwa