Rapa toka Mwanza, Coyo MC ambaye hivi karibuni ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Ziwafikie’, amefunguka kuhusu mambo aliyowahi kukutana nayo kwenye jukwaa na muziki wake.

Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Dar24, Coyo amedai kuwa maajabu ya kwanza ni mkasa uliomkuta dhidi ya promota mmoja aliyeandaa tamasha jijini Mwanza, na ya pili ni kuhusu baadhi ya matamasha aliyofanya na wasanii wakubwa wa Bongo Flava.

Alisema hatausahau mkasa wa promota aliyeandaa show yake kumtosa na kumkimbia baada ya kukusanya mapato, na shida alizokutana nazo. Kadhalika, alieleza kuhusu namna alivyowastaajabisha na kuwaogofya wasanii wakubwa wa Bongo Flava baada ya kumtanguliza jukwaani katika matamasha mkoani Mwanza.

Katika hatua nyingine, Coyo amewazungumzia Fid Q na Young Killer ambao ni wasanii wakubwa wanaowakilisha Mwanza, ambapo amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kuhakikisha anafikia na hata kuvuka kiwango cha juu cha uandishi na michano alichonacho Ngosha (Fid Q).

Angalia video hii kusikiliza yote.. usisahau ku-subscribe ili usipitwe na mengi mazuri kutoka kwenye show zetu ikiwa ni pamoja na ‘Burudani 24’.

Twiga Stars Kutajwa Mwezi Ujao
Nabil Maaloul Arejea Kuipa Makali 'Eagles of Carthage'