Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Chama Cha Wananchi (CUF) kimepeleka mashtaka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni kuwa chama hicho kimekuwa kikikiuka utaratibu wa kampeni na kuvunja kanuni na maadili ya uchaguzi, jambo ambalo CHADEMA wamelipinga vikali na kudai kuwa hiyo ni hujuma.

Hayo yamesemwa hii leo Jijini Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Saed Kubenea alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa matatizo ambayo tayari yamejitokeza kwenye chaguzi mbalimbali toka Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani yameanza kujitokeza tena kwenye jimbo la Kinondoni.

“Tunadhani Kinondoni inakwenda kuwa na shida kuliko wakati mwingine wowote kwa sababu, hiyo tukaona tuzungumze mapema ili kuondoa mambo ambayo yanaweza kupelekea shida kwenye uchaguzi. Nimeona nilete haya mambo muone kwani hawa watu tayari wana nia mbaya kuna barua mbili za malalamiko ya maadili dhidi ya CHADEMA,”amesema Kubenea

Video: Uhamiaji yawatoa hofu watumiaji wa 'Passport' za zamani
Mahakama yaingilia kati agizo la Kenyatta kuzimwa kwa vyombo vya habari

Comments

comments