Siku chache zilizopita baada ya kutokea fujo kwenye mkutano wa CUF uliokuwa umeandaliwa na upande wa wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad, upande wa pili umejitokeza na kukiri hadharani kuwa vijana waliofanya fujo katika mkutano huo walikuwa ni wa CUF.

Hayo yamesemwa mapema hii leo Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema vijana waliofanya fujo kwenye mkutano huo walikuwa ni Chama hicho.

Amesema kuwa vijana walikuwa katika doria la kawaida kwani tayari walikuwa wameshapata taarifa za mkutano huo ambao haukutakiwa kufanyika mujibu wa katiba ya chama hicho.

“Mtu yeyote asipindishe kitu, wale hawakuwa majabazi, ni vijana wetu wa CUF na walikuwa kwenye doria kwa sababu tulishasikia mikakati yao wanayoipanga na Chadema, hatuwezi kupangiwa mipango na Ukawa wakati sisi ni Chama halali,”amesema Kambaya.

Aidha, Kambaya ameongeza kuwa mchezo mchafu anaoucheza Meya wa Ubungo, Boniface Jacob na Chadema kwa ujumla wa kutaka kuisambaratisha CUF hautafanikiwa.

Hata hivyo, katika hatua nyingine, Kambaya amesema kuwa Chama Cha Wananchi (CUF),kinaomba radhi kwa waandishi wa habari, Jukwaa la Wahariri pamoja na vyombo vyao kwa tukio hilo lililolsababisha taharuki kubwa.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 26, 2017
Meya wa Jiji la Dar ahudhuria mkutano wa majiji nchini Iran