Hatimaye Chama cha Wananchi, CUF kimemaliza mgogoro wao uliokuwa ukiendelea kwa muda mrefu baina ya pande mbili zilizodaiwa kuwa CUF ya Maalim Seif na CUF ya Profesa Lipumba.

Muafaka huo umepatikana baada ya kupatikana kwa Bodi ya Wadhamini inayotambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 21, 2017, Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya amesema kuwa chama hicho kimepata Bodi mpya iliyosajiliwa na RITA na hakuna mgogoro tena kwani sasa kina bodi moja.

“Bodi hiyo inaongozwa na Peter Balebo Mwenyekiti lakini pia yupo Mkurugenzi wa Fedha Thomas Malima ambaye anakuwa kama Katibu wa Bodi. Kuna wajumbe wameainishwa, wametajwa hapa. Kwa hivyo, hivi sasa CUF Chama cha Wananchi kimekwishapata Bodi yake halali.”

BreakingNews: Trafiki wawili wapigwa risasi, gari lao lachomwa moto Kibiti
Audio: Diamond awaweka Wema Sepetu na Zari kwenye ngoma yake mpya ‘Fire’