Chama cha Wananchi (CUF) kimeshangazwa na hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuendelea kumtambua Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba kwakuwa alijiuzuru kwa hiari yake na kutimkia nje ya nchi.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Mbarala Maharagande alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kitendo hicho kinavunja Katiba ya chama hicho.

Amesema kuwa chama kimefungua kesi kwaajili ya kutaka kujua ametumia vifungu gani kuendelea kumtambua Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa amejiuzuru.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wamefungua kesi nyingine waliyofungua dhidi ya Mwenyekiti huyo ya kuhoji uhalali wa kuwafukuza uanachama wabunge wanane na madiwani wawili wa chama hicho, kitu ambacho kimesababisha taharuki ndani ya chama .

Julio apeta, wengine waenguliwa uchaguzi TFF
NASA wailaumu serikali uvamizi ofisi yao Kenya