Daktari Bingwa wa Macho na Mkuu wa Idara ya Macho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Baruani Mtemi Sufiani amesema kuwa Kope za bandia zinamadhara makubwa sana kiafya katika macho.

Dkt. Buriani amesema kope za Bandia zimetengenezwa na Kemikali ambayo husababisha muwasho katika macho kisha mikwaruzo ambayo baadaye hutengeneza vidonda ambavyo baada ya kutibiwa hubakisha makovu.

Ukubwa wa makovu hayo husababisha uoni hafifu au kushidwa kuona kabisa.

Amesema wadada wengi wanaoweka kope za bandika wakiona kuwa ni urembo bila kujua madhara makubwa yanayoweza kusababishwa na kope hizo, hivyo amewataka kuacha kutumia ili kujiepusha na madhara hayo na badala yake wabakie na kope zao.

Katika ushauri mzito alioutoa, licha ya kukataza watu kubandika kope za bandia, amesisitiza kuwa watu wakubali maumbile Mungu aliyowaumba nayo.

Dkt. Buriani amesema kumekuwa na wagojwa wengi ambao wanafika katika hospitali ya Muhimbili wakiwa na tatizo hilo na amekuwa akiwashauri kuachana na kope za bandia.

Mkurugenzi wa Chadema azidi kusota rumande
Uhuru Kenyatta: Sitobadili msimamo wangu