Katika muendelezo wa kusherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya DataVision International imetoa msaada kwa kituo cha watoto yatima kilichopo Bunju jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika utoaji wa msaada huo, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya DataVision International, Teddy Qirtu amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo.

“Katika hii miaka 20 ya DataVision tunajivunia kwa kutoa misaada mbalimbali kwa baadhi ya watu tuliowafikia na kunufaika na misaada yetu,”amesema Teddy Qirtu

Kikosi cha Simba chaanza safari kuelekea Njombe
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 2, 2018