Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) na Kampuni ya DataVision International (DVI) zimetaka wasanii wa sanaa za kazi za mikono kuunda umoja utakaowezesha kujijenga kiuchumi na kukuza kazi zao katika soko la ndani na nje ya nchi.

TAFCA na DataVision International zilikutana mwishoni mwa wiki iliyopita na wasanii mbalimbali wakiwemo waasisi wa asasi mbalimbali za sanaa kupanga jinsi ya kuwakwamua wasanii hao kiuchumi kwa kuwajenga na kuwawezesha kuendeleza vipaji vyao.

Wasanii wa Sanaa za mikono wamekuwa katika mazingira magumu ya kazi zao hali inayoplekea kushindwa kupenya kwenye hadhi ya kimataifa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na sanaa hiyo kutokuwa na umoja ambao unaweza kuwakutanisha pamoja na kupanga jinsi ya kupanua soko la bidhaa zao na kujitanua kiuchumi kuliko sasa kwa wanasanii kuonekana katika sura ya umasikini.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa TAFCA, Adrian Nyangamalle amesema kuwa sanaa ya kazi za mikono ina changamoto kubwa na kwamba hatua ya kuwakutanisha na DataVision International itawezesha kupanga jinsi ya kusonga mbele kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi.

Amesema kuwa kati ya ugumu wanaokutana nao kwenye sanaa hiyo ni kazi hizo kutozungumza kama ulivyo muziki au filamu ambazo ni rahisi kwa  mtu kujua ni nani aliyeigiza au kuimba.

“Sanaa yetu ina changamoto kubwa na kati ya changamoto zenyewe ni hizi kazi zetu kutokuimba kama wasanii wanaoimba au kuigiza ambako ni rahisi watu kujua aliyeimba au aliyeigiza ni nani, unaweza kupata jibu kwenye hili ninalosema katika mfano wa karibuni zaidi pale watu kadhaa walipojitokeza kudai ni wachoraji wa Nembo ya Taifa,” amesema Nyangamalle.

Amesema kwa sasa hali hiyo inakwenda kubadilika kwa vile wameingia katika makubaliano maalumu na DataVision International ambayo itachukua jukumu la kutafiti idadi halisi  na kuwatambua wanasanii wa kazi za mikono nchini na kupanga jinsi ya kuwasaidia kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia.

“Tunaamini kupitia kwa hawa wenzetu wa DataVision International, ambao wamekuwa kwenye wigo wa kufanya shughuli zao kwa kutumia njia mbali mbali za teknolojia tutaweza kuwatambua wasanii wote nchini na kuwawezesha nao kupata faida mbali mbali ikiwemo kazi zao kutambulika ndani na nje ya nchi., Suala letu la kujua idadi ya wasanii litakuwa rahisi na hapo wasanii wanaweza kupata thamani ya jasho lao wanalovuja juu ya kazi hizi.”

“Hii itafanya tuwafikie wasanii wote wa ndani ya Dar es Salaam na nje kuweza kufikiwa kwa urahisi, kuliko tukiendelea kukaa katika hali tuliyokaa huko nyuma” alisema Nyangamalle akiongeza kwamba sanaa ya uchongaji haiko Dar es Salaam pekee, bali iko nchi nzima, hivyo ushirikiano wao na DataVision International kuwatambua wasanii wote kwa majina, makazi na kazi zao ambazo zote zitaweza kuoneka kwenye tovuti (Web Portal) ambayo itakuwa mahsusi kwa sanaa tu hivyo kuwezesha watu na asasi mbali mbali duniani kote kujua uwezo wa wasanii wetu.

Katika hatua nyingine Nyangamalle amesema hivi karibuni alikutana naWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyehoji kwa nini sanaa za kazi za mikono hazipati kipaumbele stahiki.

Ameongeza kuwa Kampuni ya DataVision International ipo sokoni kwa miaka 18 sasa na imefanya kazi na taasisi mbali mbali za serikali na binafsi kuwezesha ufanyaji kazi kwa ufanisi kwa kutumia mbinu mbali mbali za teknolojia pia Muungano huo kati ya DataVision International na TAFCA utawezesha sanaa ya kazi za mikono kufika mbali zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya DataVison International, Kiongozi wa Kitengo cha Biashara, MacLean Geofrey amesema kuwa wanafahamu TAFCA, ina kundi kubwa la wasanii wa sanaa za mikono  ambalo halijaunganishwa pamoja na hivyo kwa pamoja TAFCA na DataVision Inernational itawaleta karibu kwa kuwatambua na kutengeneza Database ya wasanii wote nchini kasha kuwawezesha na kuwaelimisha juu ya nguvu ya Teknolojia katika kupenya katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili waweze kusonga mbele.

MacLean amewa hakikishia kuwa watamfikia kila msanii wa kazi za mikono, kujua aliko pia kuwasjili wasanii  wote na kuwapa utambulisho ili waweze kutambulika popote waendako.

“Wasanii wa Sanaa za mikono wana fursa za hali ya juu. lakini hawajakaa katika nafasi nzuri hivyo kuwapo kwetu ndani yao ni kuhakikisha kwanza tunawakusanya pamoja, tunawasajili. tukishawasajili tutafanya watambulike na hapo ndipo itakuwa rahisi kufanya kila kitu, lakini kwanza tuwasajili,” alisema MacLean akidokeza ya kuwa kati ya mikakati yao ni kufanya kazi na TAFCA kwa karibu zaidi,”amesema Macleanyao ni kufanya kazi na TAFCA kwa karibu zaidi,”amesema Maclean.

Video: Watanzania sasa kuachana na nguo za mitumba
Klabu ya Simba kukimbilia mafichoni Afrika Kusini