Kampuni ya DataVision International imeshiriki kikamilifu mashindano ya Rotary Dar Marathon ikiwa ni moja ya sehemu ya kuadhimisha miaka ishirini tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo ambapo wafanyakazi wake wameshiriki katika mbio Kilomita 42, Kilomita 21 na kutembea Kilomita 9 na 5.

Mashindano yalianza kwa wakimbiaji wa mbio ndefu kilomita 42, mbio fupi Kilomita 21, waendesha baisikeli, pamoja na watembea kwa miguu Kilomita 9 na 5 pamoja na watu wenye ulemavu.

Wakati wa kutoa zawadi kwa washindi ulipo wadia Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mh. Ally Hassan Mwinyi ndiye aliye kabidhi Medali kwa washindi wambio ndefu na fupi, na mmoja wa awakilishi wa DataVision International alipata Medali kwa upande wa mbio za Kilomita 21.

Aidha, Kampuni ya DataVision inaendelea kushiriki katika kuchangia huduma mbalimbali katika jamii ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka ishirini ya uvumbuzi na kurudisha fadhira kwa jamii kama ilivyo shiriki Rotary Dar Marathon ambayo mapato yake yataboresha huduma ya afya hospital ya CCBRT.

CCM yajitwalia Jimbo la Liwale
Trump aingilia kati sakata la kutoweka kwa mwandishi wa habari