Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema kuwa kazi yake kubwa ya kwanza ni kuhakikisha suala la Ulinzi na Usalama analipa kipaumbele, hivyo amepanga mikakati ya kuziwezesha Kamati zote za Ulinzi na Usalama kuweza kupambana na kukabiliana na makundi ya uhalifu yanayoendelea kujitokeza kila kukicha.

Ameyasema hayo leo Novemba 24, 2016 wakati akizungumza na dar24.com Ofisini kwake Temeke jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa watakaa vikao na Kamati za Ulinzi na Usalama vitakavyokuwa na lengo kubwa la kutengeneza utaratibu wa kujua taarifa za kila mwananchi anayeishi Temeke na shughuli anazofanya.

Lyaniva amesema kuwa amewaagiza Watendaji wa Mitaa na Kata kuanzisha daftari la  kujiandikisha kwa kila mtaa ili kujua taarifa na idadi kamili ya wananchi wanaoishi katika wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine ameitaka jamii kukemea na kukomesha vikundi vya uharifu kama panya road ambalo limekuwa likisumbua sana kwenye wilaya yake.

“Nataka tukomeshe kabisa makundi ya uharifu wilaya ya temeke, hasa hawa wanaojiita panyaroad, wamekuwa wakisumbua wananchi na kuwapora mali zao” Alisema Lyaniva.

Video: Makonda amsweka "rupango" mwenyekiti Gongo la mboto
Steven Gerrard Ajihukumu