Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa kukamilika kwa Hospitali ya Mama na Mtoto iliyopo Chanika, Ilala Jijini Dar es salaam kutasaidia kutoa huduma bora na nzuri kwa wananchi, kwani kutakuwa na madaktari waliobobea katika kutibu magonjwa mbalimbali.

Mjema ameyasema leo Aprili 13, 2017 Jijini Dar es salaam alipofanya ziara ya ukaguzi huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Amesema kuwa ujenzi huo unatarajia kukamilika juni mwaka huu, hivyo amewataka wananchi wa Ilala kwenda kutibiwa hapo ili waweze kupunguza msongamano katika hospitali zingine.

Akizungumza Mganga Mkuu wa Mkoa, Grace Maghembe amesema kuwa vifaa na mfumo mzima wa Hospitali hiyo umefungwa katika Teknolojia ya kisasa ambao unaifanya kuwa Hospitali ya kipekee katika Jiji la Dar es salaam itakayokuwa na huduma za kisasa zaidi, na inatarajiwa kupunguza misongamano katika Hospitali za Muhimbili, Amana na Mnazi Mmoja.

Mara baada ya kukamilika kwa Hospitali hiyo, baadhi ya huduma zitakazo kuwa zinatolewa ni pamoja na X-Ray, Upasuaji mkubwa na mdogo, kujifungua na watoto njiti.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 14, 2017
Aliyefukuzwa Granada Kuifundisha The Desert Warriors