Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameshiriki zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi  maeneo ya Kivukoni Front na kujionea wafanyabiashara mbalimbali wanaopanga bidhaa zao chini na kutoa agizo kwa Manispaa hiyo kutoruhusu mtu yeyote kutandaza bidhaa za biashara chini katika maeneo ambayo hayaruhusiwi.

Amesema hayo hayo mara baada ya kumaliza kufanya usafi  na kuongeza kuwa watu wote ambao wanaofanya biashara pembezoni mwa baraabara ya mabasi yaendayo kasi waondolewe mara moja, Mjema amesema kuna maeneo ambayo teyari yalishapangwa hivyo amewataka wafanyabiashara hao kujiandikisha nakupelekwa sehemu husika.

ACT Wazalendo wajibu mapigo ya Ole Sendeka
Video: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Wizara ya maliasili na utali