Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la wamachinga, wanaofanya bishara zao kando kando ya barabara za mabasi yaendayo kasi na maeneo ambayo hayaruhusiwi kuondoka mara moja, aidha ameongeza kuwa maeneo yaliyopangwa kwaajili ya biashara zao yapo na wanatakiwa kwenda huko na si vinginevyo.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala jijin, ameongeza kuwa maeneo hayo hayarusiwi kufanyia biashara aina yeyote hivyo wanatakiwa kuondoka mara moja na kwenda  sehemu husika na si , aidha Mjema amesema kuna utaratibu na maeneo tayari yameshatengwa kwaajili ya biashara zao.

Ameongeza kuwa Operesheni itaanza rasmi tarehe 1 mwezi ujao, maeneo yote ambayo hayaruhusiwi asionekane mtu yeyote akifanya biashara maeneo hayo ”Ni bora watii sheria bila shuruti kwa sababu atakae kaidi atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani” alisema Mjemaaaaa`

Video: DC mjema autaja mkakati wake kuhusu machinga Ilala
Lionel Messi: Guardiola Ataifikisha Mbali Man City