Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya uhalifu katika kipindi hiki hasa maeneo ya biashara na katika mitaa ndani ya wilaya hiyo.

Katika mikakati ya kupambana na changamoto hiyo Mjema ametoa rai kwa Wananchi kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kupambana na uhalifu unaoweza kujitokeza lakini pia amewaagiza Wenyeviti wa Mitaa kutambua Wananchi waliopo kwenye maeneo yao, kazi zao na wapo maeneo hayo kwa muda gani.

DC Mjema pia amezungumzia suala wa wavamiaji wa viwanja na kuwatishia Wananchi ambapo amesema Serikali ipo macho na ipo kwenye operesheni ya kuwabaini watu hao, awe ni mtu yeyote au kiongozi anayefanya uporaji huo wa viwanja Sheria itachukuliwa dhidi yake. Bofya hapa kutazama video

Picha: Meya apigwa na chakula usoni akihutubia, 'ampasua' mshambuliaji
Mhadhiri Chuo Kikuu akamatwa kwa kumkashfu Rais Magufuli mtandaoni

Comments

comments