Serikali mkoani Mtwara wilaya ya Mtwara Mjini imewaonya baadhi ya watu wanaosambaza taarifa za upotoshaji wakidai kuwa kuna baadhi ya wakulima mpaka sasa wana Korosho majumbani kwao na hawajui lini watauza kwa kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Evod Mmanda wakati wa kikao na wakulima wa Kata ya Naliendele ambao wamedai Korosho hizo zinazozungumziwa hazina Ubora na zimekataliwa zaidi ya mara mbili baada ya kukaguliwa kwenye Maghala Makuu.

 Akizungumza na wakulima ambao ni wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika Naliendele Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa ameona taarifa kwenye Moja ya Chombo cha Habari juu ya wakulima wa Kata hiyo inayodai kuwa mpaka sasa bado wana Korosho ambazo ziko Majumbani na hazijauzwa hatua iliyomsukuma kutaka kujua ukweli wa jambo hilo.

 ”Ndugu zangu nilivyokua nafuatilia Taarifa ya Habari nikaona Mnadai mna Korosho na Hamjui lini Mtauza sasa nimekuja hapa nataka kujua hizo Korosho imekuaje ziwe Nyumbani, kwani Msimu Umefungwa au kuna alieleta Korosho hapa kwenye Chama chenu cha Msingi cha Ushirika akakataliwa kwamba serikali imesitisha kununua?, Sasa nimekuja nataka kusikia moja kwa moja kutoka kwenu mniambie imekuaje lakini kabla sijawasikiliza katibu wa Naliendele AMCOS haya niambie unafahamu nini kwenye hili,”amesema DC Mmanda

Aidha, kwa upande wake Katibu wa Naliendele AMCOS, Hakina Muhidini amesema kuwa Korosho hizo zinazo zungumziwa zilishafikishwa kwenye chama hicho na zikapimwa lakini baada ya kupelekwa kwenye Maghala makuu ambapo kuna wataalam wa vipimo zikaonekana hazina Ubora kulingana na Madaraja yanayo takiwa.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wamesema kuwa taarifa hizo ni za kweli lakini kilicho washangaza ni kuona Korosho hizo kuonekana hazina Ubora wakati wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuziweka katika Madaraja wanayo amini yanafaa ukizingatia kilimo cha Korosho ndio kazi iliyo walea.

Hata hivyo, kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya hiyo amewataka wakulima hao kuendelea kufuatilia na kutekeleza maagizo, Maelekezo na miongozo mbalimbali inayotolewa na viongozi wao pamoja na Serikali akisema twaratayari zoezi la uhakiki kwa asilimia kubwa limekamilika kilichobaki ni kumalizia malipo ambayo nayo kwa asilimia kubwa wakulima walio wenyi wamesha lipwa na kasi iliyopo inaridhisha.

 

Video: Makonda afanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Reli Mpya
Video: Wakali wa kolabo WCB, wavunja rekodi nyingine na 'Tetema', Tazama

Comments

comments