Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz anayefanya vizuri katika sanaa hiyo ameachia ngoma yake mpya na mwanamuziki wa kimataifa Omarion ijulikanayo kama Africana Beuty.

Siku za karibuni Diamond alipata pigo baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kumfungia nyimbo zake mbili ambazo alifanya na wasanii wa mataifa, Waka waka aliyofanya na Rick Ross pamoja na halleluyah aliyofanya na Morgan Heritage.

Kufuata sakata hilo Diamond alipohojiwa nchini Kenya akifanya ziara ya uzinduzi wa albamui yake ya A boy from Tandale amesema akirejea nchini atatafuta muda wa kuongea na Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kuweka baadhi ya mambo sawa.

Aidha ameikumbusha Serikali ya Tanzania kuwa dunia imebadilika kulingana na ukuaji wa teknolojia na utandawazi, hivyo kama wasanii wanakimbizana na utandawazi huo ili muziki wao usiwe nyuma lengo ikiwa ni kuifikisha Bongo fleva kimataifa.

Kuutazama muziki huo, bonyeza linki hapo chini.

TMA yakanusha taarifa za Tanzania kukumbwa na kimbunga
Video: DataVision, MacLeans BeneCIBO zarudisha tabasam la mtoto Mariam