Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Nassib Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz amekiri kuwa mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobeto ni wake hivyo amesema kuwa hakuna haja ya kuendelea kuongelea uhusiano huo mitandaoni.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na kituo cha Redio cha Clouds jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Diamond amesema mama yake alitukanwa katika mitandao ya kijamii baada ya kumtembelea mwanamitindo huyo alipojifungua takribani wiki sita zilizopita.

“Nilimwomba mama yangu aende akamwangalie mtoto ingawa hakuwa amefurahishwa na tukio zima, nilimwambia mama yule ni mtoto wangu hana jinsi inabidi tu akamwangalie lakini alipokwenda mwenzangu aliwaita watu wampige picha na baadaye alidhalilishwa mitandaoni,” amesema Diamond.

Diamond amesema mbali na mama yake tukio hilo limemdhalilisha mzazi mwenzake kwa kuwa picha na video zilizokuwa zikitolewa zililenga kumuumiza,

“Zari hana hatia katika hili, haya yote yanatokea kwa sababu ya ujinga wangu, maskini yangu wote wameingizwa katika mkumbo na kudhalilishwa, namshukuru Mungu nilimweleza ukweli wote mzazi mwenzangu naye akanielewa,” amesema Diamond.


Gigy Money ataja sababu ya 'Papa' kufanya vizuri
Mbunge Musukuma na wenzake wapandishwa kizimbani