Mwanamuziki Diamond Platinumz na timu yaa WCB leo wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda madawati 600 kwa ajili ya kumuunga mkono Mkuu huyo wa mkoa kukabiliana na changamoto zinazokabili sekta ya elimu.

WCB walitoa ahadi ya kumkabidhi Makonda ambaye ni mlezi wao, zawadi kwa ajili ya Watanzania, na leo wametimiza ahadi hiyo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Akizungumza katika tukio hilo, Diamond amesemshukuru Makonda kwa kukubali kuwa mlezi wa timu yao na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa watanzania kama sehemu ya kurudisha katika jamii.

“Siwezi kusema kuwa ni kikubwa… ni kidogo tulichokileta, tumeleta madawati 600 kwa ajili ya mkoa wa Dar es Salaam. Kwa sababu tunaamini kuwa kuna watu wanatusapoti mpaka kufika hapa. Kwa kidogo tunachokipata tutakuwa tunakirudisha katika jamii,” alisema Diamond.

Alieleza kuwa wameanza na Mkoa wa Dar es Salaam lakini baadae wataendelea katika mikoa mingine nchini kadri watakavyojaliwa.

Lowassa: Ninasononeshwa na hali ya Watanzania hivi sasa
Video: Maelezo ya Kamanda Msangi Kuhusu Majambazi 3 Kuuawa Mwanza