Nyota wa Bongofleva Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz  amezindua bidhaa yake mpya aliyoipa jina la Diamond Karanga ambayo itapatikana katika maduka yote nchini Tanzania.

Diamond amezindua bidhaa hiyo kwa ‘show kali’ kwa mashabiki wake na wote waliokusanyika kushuhudia uzinduzi huo, ambapo baada ya hapo alizindua rasmi bidhaa yake na kuweka wazi gharama ya Karanga hizo kuwa ni shilingi mia tatu tu (300) ambayo kila mtu atamudu kununua.

Kabla ya Diamond kuzindua bidhaa hiyo ya Karanga, hivi karibuni alizindua bidhaa manukato ya Chibu Perfume ambayo tayari ipo sokoni.

Dani Ceballos Azua Jambo Santiago Bernabéu
AFC Bournemouth Yamng'oa Nathan Ake