Katika kikao kilichofanyika baina ya Waziri wa Habari, Sanaa , Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Naibu wake, Juliana Shonza na msanii wa nyimbo za bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz, kimefanikisha kuondoa tofauti iliyokuwa kati ya Wizara hiyo na Diamond.

Ambapo Kufuatia kikao hiko Mwakyembe alimtunuku rasmi Diamond, ubalozi wa maadili ya kazi za sanaa kutokana na kuwa watu na wasanii kwa ujumla wanamuangalia Diamond kama kioo.

Hivyo Diamond hakusita kukubaliana na jukumu hilo na mbele ya viongozi wote waliohudhuria kikao hiko kilichofanyika kwenye ofisi za Waziri jijini  Dar es salaam, ameahidi kuwa atashirikiana vizuri na uongozi mzima kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano bora kwa wasanii na nchi nzima ili kulinda utamaduni wa Tanzania.

”Diamond ni balozi utake usitake, na safari hii tumemwomba sasa hata maadili awe balozi wetu, sababu Diamond ni Superstar tunajivunia watanzania” amesema Mwakyembe.

Mchakato huo ni kufuatia nyimbo za wasanii wa muziki wa bongo fleva kufungiwa kwa madai ya kukosa maadili ya kitanzania zikiwemo nyimbo mbili za Diamond, pamoja na Roma Mkatoliki kufungiwa kujihusisha na kazi za sanaa kwa muda wa takribani miezi 6, hali iliyopelekea Daimond na Naibu Wziri, Juliana Shonza kurushiana maneno juu ya maamuzi hayo yaliyofanywa na wizara hiyo dhidi ya wasanii.

Hatimaye: Nyimbo 15 zilizofungiwa zafunguliwa rasmi kwa masharti
Diamond afikia maridhiano na Serikali, 'maadili kwanza'

Comments

comments