Msanii wa Bongo fleva hapa nchini, Nasibu Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz ametoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa Said, kijana aliyetobolewa macho na Scorpion, Diamond ametoa msaada huo na kuwaomba wasanii na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia kijana huyo kwani matatizo huwa yanatokea kwa mtu yeyote.

‘’Nimeguswa ndio maana nimekuja kutoa msaada huu kutoa ni moyo na wala sio utajili, hawa ni wadau wetu  katika tasnia yetu ya muziki, nawaomba wadau na wasanii wajitokeze’’ alisema Diamond.

Kwa upande wake Said amemshukuru msanii huyo na kusema kuwa ni shabiki mkubwa wa msanii huyo na kuongeza kuwa alikuwa na ndoto siku moja ya kukutana na msanii huyo na kusema kuwa kwa sasa hivi anakosa kuziona video zake na kubaki kusikiliza video tu.

Makonda atimiza ahadi yake kwa kijana aliyetobolewa macho na Scorpion, kununuliwa nyumba, pikipiki 5 na bajaji 2
Liverpool, Man Utd Zatahadharishwa Mapema