Msanii wa muziki nchini, Diamond Platinumz amemkana mama mtoto wake Hamisa Mobetto mbele ya mama yake mzazi Bi Sandra Katika usiku wa Aunty Ezekiel kwenye uzinduzi wa filamu ya Mama aliyofanya na mwanaye Cookie Iyobo uliofanyika jana jijini Dar es salaam eneo la Mlimani City.

Diamond amesema hawezi kwenda na mama mtoto wake huyo kutokana na kuwa Hamissa Mobeto sio mama yake mzazi hivyo kwa siku ya jana alipendezwa kwenda na shujaa wake ambaye ni mama yake kutokana na siku hiyo kuwa siku ya kina mama duniani.

Diamond amesema hayo pindi alipoulizwa ni kwa nini hakwenda na mama yake mzazi katika hafla hiyo.

Aidha Hamisa Mobetto naye amefanya mahojiano na waandishi wa habari amedai kuwa anawashukuru baba watoto wake kwa majuku wanayoyachukua ya  kuwatunza vyema watoto wao hivyo ina mpa ujasiri wa kutokujiita single mom yaani mzazi mmoja.

Tazama video hapa chini kwa kubonyeza kitufe chekundu ili kumtazama Diamond Platinumz akifanyiwa mahojianao hayo.

Massimiliano Allegri aikana Arsenal hadharani
Roberto Mancini ajitwisha zigo la Italia

Comments

comments