Kufuatia kusambaa kwa picha na video mbalimbali za msanii wa Muziki wa Bongo Fleva na Rais wa Wasafi Classic Baby, Diamond Platinumz, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema mwanamuziki huyo jana alishikiliwa na polisi kwa mahojiano juu ya video na picha hizo zilizokosa maadili katika mtandao wa kijamii.

Lakini pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la polisi kumkamata kwa mahojiano mwanamuziki Nandy ambaye siku chache zilizopita video yake akiwa faragha na msanii mwenza, Bill Nas ilivuja na kuibua mtafaruko, ambapo watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki walizungumzia swala hilo kwa namna tofauti.

Aidha Diamond naye kwa siku ya jana katika mitandao yake ya kijamii kumekuwa na video mbalimbali zilizokuwa zikimuonesha yupo chumbani na wanawake wawili tofauti, hali ambayo imetafsiriwa tofauti na mashabiki zake huku wengine wakidai kuwa anawadhalilisha wanawake.

” Tunaangalia namna ya kuwafikisha Makahamani wasanii Diamond na Nandy kutokana na kusambaza mitandaoni video zisizo na maadili” Dkt Harrison Mwakyembe.

Hata hivyo matukio ya wasanii hao yanahusishwa na kile kilichopostiwa na January Yusuph Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais  anayeshughulikia Muungano na Mazingira katika Serikali ya Awamu ya Tano ambaye alitumia ukurasa wake wa Twitter kuandika haya.

”Kwa wadogo zangu maarufu kaka na dada: Umaarufu ni jukumu, litumikie kistaarabu, linaweza kudumu kwa dakika 15, muda unaotutosha kabisa kwa sisi kukufurahia au kukuchukia, na kuendelea. lakini pia ni jukumu linaloweza kuishi milele, na kuhakikishia uzima. Au jukumu linazoweza kuishi kiasi cha kukuharibia ”.

 

Diamond akamatwa, ahojiwa kwa video za faragha
Mkuchika awatahadharisha viongozi wanao wabania Walimu

Comments

comments