Mkurugenzi Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba amechukizwa vikali na tabia ya baadhi ya wasanii iliyozuka hivi karibuni ya kutumia ovyo mitandao ya kijamii kwa kurusha picha za utupu.

Amewataja wasanii hao wanautumia vibaya mitandao ya kijami na kusema BASATA inabidi ichukue hatua kali dhidi ya wasanii ambao wanaharibu vizazi vijavyo.

Amewataja wasanii hao ni Diamond Platinumz, Nandy, Amber Ruthi, Amber Lulu, Wema Sepetu, Sanchoka, Hamissa Mobeto, Gigy Money na kurasa nyingine nyingi za Instagram zinazotumika vibaya kuweka picha zisizo na maadili.

”Diamond Platinumz, Amber Ruth na Wema Sepetu walitakiwa wawe gerezani, mimi nina watoto wakike watano, inasikitisha sana” Amesema Musiba.

Amehoji Baraza la Sanaa Tanzania kuwa hawa watu wanaharibu kizazi kijacho inakuwaje wanasemehewa.

Sikiliza hapa chini.

Bilionea klabu ya Leicester City FC afariki dunia
Video: Zitto aibua tuhuma nzito za mauaji, Kutekwa Mo kulivyobadili upepo

Comments

comments