Diwani wa Kata ya Kunduchi iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, Michael Urio ameahidi kuwasaidia mahitaji yao wahitimu wa mafunzo ya ufundi Cherehani waliomaliza katika taasisi ya Nubosco.

Aidha, Diwani huyo ameipongeza taasisi hiyo kwa huduma nzuri ya kuisaidia jamii, hivyo amewaasa wadau mbalimbali kuiga mfano huo.

“Niwaahidi kitu kimoja ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwenu, nawaomba mfike ofisini kwangu muunde vikundi ili tuangalie utaratibu wa kuwakopesha mjiajiri kwasababu tayari ujuzi mnao,”amesema Urio

 

 

Watunisia kuandamana kupinga ugeni wa Mwana wa mfalme wa Saudi
Msigwa apigwa kitanzi tena

Comments

comments