Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa vyama vya siasa vinatakiwa kuiga mfano wa taasisi za kidini ambazo zimekuwa na ushirikiano wa hali ya juu.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza katika mkesha wa Maulid ya kuzaliwa mtume s. a. w, ambapo amesema kuwa viongozi wa dini wameonyesha mfano mzuri na unatakiwa kuigwa na vyama vya siasa ambavyo siku zote vimekuwa vikitengana hasa linapotokea janga la kitaifa.

“Kila siku nimekuwa nikijifunza, kwakweli katika ushirikiano huu wa taasisi za dini umenipa faraja sana, huu ni mfano ambao vyama vya siasa hapa nchini vinatakiwa kuiga, ushirikiano mkubwa kabisa nimeuona dini mbali mbali zipo hapa leo, lakini nawaomba sana mzidi kutuombea sisi wanasiasa,”amesema Dkt. Bashiru

Hata hivyo, Dkt. Bashiru ameongeza kuwa kama vyama vya siasa vikiondoa masuala ya tofauti za itikadi na kushirikiana, basi Tanzania itapiga hatua kubwa katika suala zima la maendeleo.

Luis Suarez: Dembele bado ana nafasi FC Barcelona
Hispania, Ureno kuishawishi Morocco 2030