Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipaswa aliongelee hadharani suala la kifo cha mwanafunzi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT).

Amesema kuwa jambo hilo ni kubwa na zito hivyo haiwezekani kutuma salamu za pole kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Hili jambo ni kubwa sana na linamgusa kila mtu, sidhani kama ni sahihi kwa Rais Dkt. Magufuli kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kutoa maagizo na pole kwa familia ya Akwilina, sina uhakika kama yule Baba mzazi wa mtoto huyu kama ameupata ujumbe wa Rais,”amesema Bisimba

 

Ndalichako abeba jukumu la Akwilina, ahaidi kumsomesha mdogo wake
Padri akiuka miiko ya kikatoliki, atangaza ndoa

Comments

comments