Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha LHRC, Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amekanusha taarifa ambazo zimezagaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa ameteuliwa kujiunga na baraza la wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa hajapokea taarifa yeyote kutoka Chadema hivyo hawawezi kutangaza kitu kama hicho bila ya kumuuliza.

Amesema kuwa taarifa hizo ni za uzushi na wananchi wanapaswa kuzipuuza kwani yeye hana sifa za kuwa mwanasiasa na hata kama angechaguliwa asingekubali kuwa miongoni mwa baraza la wazee wa Chadema.

“Taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimechaguliwa katika baraza la wazee wa Chadema ni uongo, na hata kama ningechaguliwa nisingekubali,”amesema Dkt. Hellen Kijo- Bisimba

Video: Mhagama kula sahani moja na Mwalimu 'Mpapasaji' wa wanafunzi
Kesho Ndugai kutaja kamati za kuchunguza gesi na uvuvi