Mkurugenzi wa Kituo Cha Haki za Binadamu LHRC,  Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amelaani kitendo alichokifanya Mwalimu wa shule ya St. Florence cha kuwadharirisha watoto wa kike.

Ameyasema hayo Jijini Dar e salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa jambo hilo ni la kukemea kwani watoto wanapaswa kupata ulinzi.

Amesema kuwa kitendo hicho ni uvunjifu wa haki ya mtoto wa kike pia uvunjifu wa maadili ya waalimu ambapo ameongeza kuwa kitendo hicho kimeshusha hadhi ya waalimu.

“Mwalimu anapaswa kumpa ulinzi mtoto na kuhakikisha kuwa hapatwi na tatizo lolote, na kuto kumvunjia haki zake za msingi,”amesema Dkt. Bisimba

Video: Uozo gesi asilia, uvuvi kuanikwa, Lissu aamsha dude bungeni
Magazeti ya Tanzania leo Juni 2, 2018