Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameagiza makontena 20 ya samani yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yapigwe mnada ikiwa ni sehemu ya kusimamia sheria na kanuni za kodi zilizopo nchini.

Ametoa maagizo hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na kukagua makontena hayo katika Bandari Kavu ya (DICD).

Aidha, Waziri Mpango ameweka wazi kwamba hajali vitisho vya mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam na ameapa kuendelea kusimamia sheria na kanuni za kodi nchini na hilo halichagui mtu wala nafasi yake.

Akiwa kwenye ibada jana huko Wilayani Ngara mkoani Kagera, Paul Makonda alitoa onyo kwa mtu atakayenunua makontena hayo  yenye samani za ndani kama vile meza, viti na mbao za kufundishia atapata laana lakini Waziri amesema hatojali vitisho hivyo.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 28, 2018
CAF yaridhishwa na maandalizi ya AFCON