Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango leo amezindua tawi jipya la Benki ABC  lililopo Tegeta Jijini Dar es salaam na kuwataka wananchi kuitumia vizuri huduma hiyo waliyosogezewa.

Aidha, Dkt. Mpango amewaasa wananchi wasiogope kukopa kwani mikopo itawasaidia kujiendeleza kimaendeleo, na amewataka kurudisha mikopo yao kwa wakati ili kuweza kujenga uaminifu wa kukopeshwa mara nyingi zaidi.

“Wananchi tumieni fursa hii mmebahatika kuwa nayo, lakini wengine hawana huduma ya tawi kama hili jipya, litumieni muweze kujikwamua kiuchumi na maendeleo,”amesema Dkt. Mpango.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 30, 2017
University of Phoenix Online What a Joke!