Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka Bodi ya Bima kurejesha kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) waliyokaa nayo kwa muda wa miaka saba.

Dkt. Mwakyembe amefikia hatua hiyo mara baada ya kufanya ziara katika Ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), na kujione hali mbaya ya majengo ambayo ilipelekea kuhoji uharali wa baraza hilo kukaa kwakujibana kwenye majengo yaliyochakaa.

Aidha baada ya kusomewa taarifa ya uendeshaji wa ofisi hizo  ilibainika kuwa kuna kiasi kikubwa fedha ambazo zimehifadhiwa Bima kwa muda wa miaka saba, hivyo kuiamuru mara moja Bodi ya Bima kuzirejesha fedha hizo kwa baraza hilo ili liweze kujiedesha lenyewe.

“Nataka niseme kwa nataka umwambie Mwenyekiti wa Bodi ya Bima warejeshe hiyo pesa mara moja, kwanini wamekaa nazo, na kama wakishindwa mimi ntafurahi sana maana najua ni wapi pa kuwabana, haiwezekani mkajibana bana hivi hapa,”amesema Dkt. Harrison Mwakyembe.

Hata hivyo, katika ziara yake hiyo Dkt. Mwakyembe amemtaka Mkurugenzi wa Bakita kuwasiliana na Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ili kikao cha dharula kifanyike kwa haraka zaidi cha kuangalia namna ya kuzirudisha fedha hizo.

Video: Dkt. Mwakyembe awaweka mtegoni BAKITA
Mke wa Mugabe awaponyoka polisi Afrika Kusini na tuhuma za kumpiga mrembo