Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika kutoa huduma za afya ingawa bado kuna changamoto kwa upande wa vifo vya kina mama.

Amesema kuwa kwasasa wanakabiliana na changamoto ya vifo vya kina mama, hivyo serikali imepanga kutoa elimu ya kutosha mijini na vijijini.

Aidha, ameongeza kuwa vifo kwa akina mama wakati wa kujifungua havikubariki kwani ujauzito si ugonjwa hivyo serikali itapambana na changamoto hiyo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo pamoja na mengine amesema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha inaondoa changamoto mbalimbali za kiafya.

Video: TPSF kufungua milango ya fursa za uwezekezaji nchini
Video: Mkuu wa mkoa azua kizaa zaa, Mabilioni ya Barrick ngoma nzito

Comments

comments