Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Kigamoni, Dkt. Faustine Ndugulile amzindua kampeni ya zimamoto mlango kwa mlango Kigamboni jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi.

Uzinduzi huo umefanyika hii leo Kigamboni jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuepukana na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiikumba jamii.

“Kampeni hii lengo lake ni kutoa elimu kwa wananchi ambao wamekuwa waathirika wakubwa katika majanga ambayo yamekuwa yakitokea,”amesema Dkt. Ndugulile

Video: Ukiivuruga Serikali unalala na njaa- Musiba
Video: DC Mgandilwa afichua danguro la kusafirishia mabinti Uarabuni