Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa amesema kuwa atafanyakazi kwa juhudi na uwezo wake wote ili kuisadia serikali kuweza kusonga mbele katika suala la maendeleo.

Ameyasema hayo hii leo Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kuapishwa, ambapo amemuahidi Rais Dkt. Magufuli kuwa hatomwangusha katika utendaji kazi wake.

Adha, Dkt. Slaa amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa balozi kwani amesema alikuwa na kiu kubwa ya kuitumikia nchi yake

“Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakushukuru sana kwa kuniona na kuniteua kuwa balozi, kiu yangu kubwa ilikuwa ni kuitumikia nchi yangu,”amesema Dkt. Slaa

Hata hivyo, Dkt. Wilbrod Slaa ameapishwa hii leo jijini Dar es salaam, huku kituo chake cha kazi kitakuwa nchini Sweden.

Chadema yakanusha kususia uchaguzi
Rungwe, Chadema waiwashia moto CCM