Abdulaziz Chande maarufu kwa jian la Dogo Janja ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Banana’ ngoma hiyo ni majibu ya kile ambacho kilizuka mtandaoni siku chache zilizopita, ambapo Dogo Janja kupitia mtandao wake wa instagram alimhoji mke wake, Irene Uwoya endapo anataka banana naye Irene akajibu anataka “Cassava”, ujumbe uliozua mahojiano mengi mtandaoni.

Kumekuwa na stori nyingi za wana ndoa hao hivi karibuni hali iliyofanya kuwaibua baadhi ya wasanii wengine ambao walizungumza tofauti tofauti juu ya maisha ya wanandoa hao.

Moja ya watu waliosema chochote kwa wawili hao ni mwigizaji, Mwijaku ambaye alichukizwa na kitendo cha Irene Uwoya kurusha mtandaoni picha zilizoonyesha baadhi ya maumbile yake na kusema kuwa Dogo Janja hana sauti katika ndoa yake.

Hata hivyo, msanii Shamsa Ford naye aliibukia sakata hilo na kusema kuwa alichofanya Irene Uwoya ni sawa kulingana na mazingira aliyopo lakini pia ni kitu ambacho kinafanyika hata na mastaa wakubwa huko Marekani.

Aidha, ndoa ya Dogo Janja imefikisha miezi tisa na siku kadhaa, tangu wawili hao waoane.

Katika Wimbo wa Banana Dodo Janja kuna mashairi ambayo huenda ni vijembe kwa watu wote ambao hawana imani na ndoa yake. Bofya hapa kuusikiliza wimbo huo.

 

 

 

Cavani, Suarez wazima ndoto za Ronaldo kombe la Dunia
Marcelo Vieira da Silva Júnior aumiza vichwa madaktari

Comments

comments