Msanii wa bongo fleva nchini chini ya lebo ya Tip Top Connection, Abdulaziz Chende maarufu kama Dogo Janja toka Ngarenaro ambaye kwa sasa ni mume wa msanii wa filamu za bongo, Irene Uwoya ameachia kibao kipya kinachoenda kwa jina la Wayuwayu.

Wimbo huo umefanywa kwa ubunifu mkubwa ambapo Dogo Janja ameonekana kwa namna tofauti tofauti na mpaka sasa ni moja kati ya nyimbo zinazofanya vizuri katika mtandao wa You Tube na kupelekea kushika nafasi ya tatu kwa kutazamwa na watu wengi.

Mashairi ya wimbo huo yanaonekana yakimuhusu moja kwa moja mke wake, Irene Uwoya kutokana na kile kilichosikika kikiimbwa katika wimbo huo.

Janjaroo amesikika katika mashairi yake akiimba kuwa ”Mtoto jicho kungu manga, wala hautoki Tanga, hata nikiwa na njaa huwa nawaza kukumanga”.

Ameongezea ”Wakija kwako na maneno musururu, wanakwambia natumia putururu, wote wambea waoga ka kunguru, lakini bahati mbaya mdomo hatulipi ushuru”.

Tangu kuachiwa kwa wimbo huo masaa 24 yaliyopita imetazamwa na watu 50,228.

Kusapoti kazi za ndani na kumsapoti kijana mdogo anayefanya vizuri kwenye sanaa ya muziki bonyeza link hapo chini kuutazama.

Wanaharakati watatu wahukumiwa miaka 10 jela
DC Hapi awafukuza ofisini wabunge wa Chadema

Comments

comments