Kampuni ya DataVision International  imetoa wito kwa vikundi vya SACCOS, VICOBA na Taasisi mbali mbali za kifedha kutokubaki nyuma katika mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi na kuendelea kufanya kazi kwa mazoea. Katika Maonyesha ya Kifedha yaliyofanyika katika kumbi za Diamond Jubilee, kampuni ya DataVision iliweza kuwaonyesha watu waliotembelea banda lao mifumo yao mipya ambayo inaweza kuongeza ufanisi katika sekta hio.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Novemba 10, 2016 katika maonyesho ya Taasisi za kifedha Diamond Jubilee Dar es salaam, Meneja Masoko wa Datavision International , Teddy Qirtu amesema “Makampuni katika sekta ya kifedha yanayakiwa kubadilika na kwenda kwa spidi ambayo mabadiliko ya kiteknolojia yanakwenda. Aliongezea pia wamekuja na mfumo mpya wa “KadiPap!” ambao huwezesha taasisi mbali mbali ikiwemo za kifedha kuwapa kadi za ATM wateja wao papo hapo. Imezoeleka sana watu kusubiri kadi kwa zaidi ya hata wiki katika sekta hii ambayo imekuwa ikileta kero kwa wateja, ila na mfumo huu mpya unahakikisha kuwa matatizo hayo hayatatokea tena.

Bofya hapo chini kutazama video hii.

Fabio Capello Afichua Siri Ya Kuikataa The Azzurri
Video: Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu miongozo na viwango vya TEHAMA