Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema uwepo wa dini umewezesha nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu hivyo kila mmoja ahakikishe suala hilo linaendelezwa.

Majaliwa ametoa wito huo leo Novemba 18, 2016 wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo amewasihi waislam kuimarisha umoja, upendo na mshikamano miongoni mwao kwa kushirikiana na jamii zinazowazunguka bila kujali tofauti zao za kiimani.

Pia amewashauri waumini na viongozi wa dini kuzingatia maadili ya dini ili kuepusha migongano isiyo ya lazima hasa taasisi zinapokuwa na miradi.

 

Video: Gereza la keko lapigwa faini ya mil. 30
Video: Majaliwa afanya ukaguzi ujenzi wa Magomeni Kota, Ataka ukamilishwe kwa wakati