Zaidi ni kipindi ambacho kinaruka kila siku ya jumatatu ambapo tunakuletea mambo mbalimbali yaliyowahi kuvunja rekodi duniani.

Leo Julai 16, 2018 tunakujuza migahawa 6 inayotoa huduma za ajabu duniani ambapo moja ya mgahawa maarufu nchini China ni ”Guolizhuang Restaurant” unaopatikana katika mji wa Beijing ambapo katika mgahawa huu chakula pekee kinachohudumiwa ni sehemu za siri (uzazi) za wanyama mbalimbali.

Na raia wa China wanaamini kuwa sehemu za siri za wanyama husaidia kuongeza nguvu na uwezo wa mwanaume kuzalisha huku pia humsaidia mwanamke kulainisha ngozi yake.

Hata hivyo unaambiwa moja ya kiungo cha siri kinachouzwa kwa gharama kubwa katika mgahawa huo ni uume wa mnyama ajulikanae kama chui ambapo gharama zake zimetajwa kuwa ni dola 1500 za Marekani ambayo ni sawa na Milioni 2.5 kwa pesa za kitanzania.

Bofya hapa kufahamu na kuwa wa kwanza kutazama huduma nyingine za ajabu zinazotolewa katika migahawa tofauti hapa duniani.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 17, 2018
Video: Wema Sepetu awaomba watanzania wamuombee

Comments

comments