Ikiwa leo ni Februari 14, 2019 ni siku maalum ya kuoneshana upendo, ambapo siku hii watu hupeana zawadi mbalimbali kama ishara ya mapendo, siku hii ilianzishwa rasmi na mtakatifu Valentino aliyeuawa na mfalme huko Italy, Roma karne ya 14 mara baada ya kukaidi agizo lake la kufungisha ndoa.

Mtakatifu Valentino aliona ni vyema watu kufunga ndoa ili kupunguza matendo ya uzinzi.

Siku ambayo Mtakatifu aliamriwa kunyongwa, kabla ya kutekelezwa hukumu hiyo, Mt. Valentino aliomba kalamu na karatasi ambapo aliandika ujumbe mzuri kwa mpenzi wake bintiye Afisa wa Magereza.

Mwisho wa ujumbe huo alimaliza kwa kuandika ”From your Valentine” ilikuwa Februari 14 ndiyo siku ambayo mtakatifu Valentino alinyongwa nakuaga dunia.

Nchi mbalimbali husherekea siku ya wapendanao kwa namna tofauti tofauti, kama kumbukumbu ya mtakatifu Valentino aliyekubali kufa kwa ajili ya kudumisha upendio.

Fahamu nchi hizi jinsi zinavyosherekea siku hii ya wapendanao ”Valentines Day”.

Majaliwa aipa neno benki ya NBC, 'Sasa ongezeni wigo'
Naibu waziri Ikupa ahimiza ushirikiano