Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameitaka kampuni ya Nyanza inayoshughulikia ujenzi wa barabara ya mkoani Kigoma kuanza kufanya kazi usiku na mchana kwa kuwa wapo baadhi ya wananchi hawajahi kuona lami maisha yao yote mpaka wanakufa.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akihutubia wakazi wa Kakonko mkoani Kigoma katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo mpaka Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami.

“Wananchi hawa wanahitaji barabara ya lami wameteseka tangu dunia iumbwe, wako watu hawajui rangi ya lami, wapo watu hapa wamezaliwa, wamezeeka hawajui rangi ya lami ikoje. Kwa sababu hawajawahi kuona barabara ya lami katika maisha yao, kwa hiyo nataka hii lami ianze na mjipange kweli mfanye kazi usiku na mchana”, amesema Rais Magufuli

Aidha, amesema kuwa kwa bahati nzuri anauzoefu mkubwa wa kuwafukuza kama anakunywa chai na kutoa tahadhari kwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo kuwa kwa sasa yeye ndiye baba wa wote

Mahakama Kuu yaamuru Tigo kuwalipa AY, FA Tsh Bilioni 2.1
Majaliwa atoa neno kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi