Klbu Bingwa nchini Ujefrumani FC Bayern Munich imetwaa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA), kwa kuwafunga mabingwa wa Ufaransa PSG bao moja kwa sifuri.

Bao la ushindi la FC Bayern Munich lilifungwa na mshambuliaji kutoka Ufaransa Kingsley Coman, dakika ya 59 kipindi cha pili.

Washambuliaji PSG Neymar, Mbappe na Di Maria walishindwa kutumia vema nafasi walizozipata katika kutawala mpira na kupelekea Bayern Munich kuitumia nafasi hiyo na kutawala mpira karibia dakika zote za mpira.

Hata hivyo Mlinda mlango wa Bayern Manuel Never alifanya jihada kubwa kuzuia hatari zilizokuwa zikifanywa na Neymar, Mbappe na Di Maria.

FC Bayern Munich imefiisha idadi ya mataji sita ya barani Ulaya, wakifanya hivyo mwaka 1974, 1975, 1976, 2001, 2013 na 2020.

Belarus : Wapinzani wataka Rais aachie madaraka
Askari Polisi mbaroni kwa kumbaka mtoto wa miaka minne – Kenya