Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Kasheku Msukuma amesema kuwa fedha za ruzuku za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zinagawanwa na wabunge watatu wa chama hicho ambao amewataja kuwa ni Freeman Mbowe, Godbless Lema na Halima Mdee.

Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa fedha hizo zimekuwa zikiishia mikononi mwa wabunge hao.

Amesema kuwa chama hicho hupewa ruzuku ya shil. 420 milioni kwa mwezi huku kila mbunge wa Chadema huchangia shilingi mil.1.8 kwaajili ya kuimarisha chama.

“Sisi tukizungumza tunajua siri na ni haki yangu kama mbunge kuzungumzia hili, mtu akiwa ndani ya Chadema haruhusiwi kuhoji na akihoji anafukuzwa kwa kuonekana msaliti,”amesema Msukuma

 

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 8, 2018
Video: Polisi feki wakamatwa Jijini Dodoma wakikusanya mapato

Comments

comments