Mkubwa Fella ambaye ni miongoni viongozi wa WCB amempa onyo msanii wa muziki kutoka kwenye lebo hiyo, Mbosso kuhusu ushawishi anaopata kutoka kwa watu ili ajitoe.

Mkubwa Fella aliweka picha ya Mbosso katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika; “Nasema mwanangu Mbosso piga kazi kumbukizi zisikulazimu kumuonea huruma utakaye kutana nae jukwaani pambania kumkalisha utakae muona ila tanguliza bendera ya nchi yetu ya Tanzania pia uza brand yako WCB Wasafi.”

”Ila nakusihi unaenda kwenye ukubwa sasa wasijitokeze wanao kushawishi ujitoe kumbuka mkataba mwanangu, muda huu wanajifanya kama hawakuoni tunapambana sisi tu Kwenye ukuwaji wako Mkubwa Fella, diamond Platnumz, Babutale na Sallam ila baadae wanajitokeza wanao kuona biashara sasa Mwanangu wakija kukushawishi wakumbushe una mkataba.”

“Wakiweza waje wasije wakakurubuni baadae tukiwambia gharama za ukuaji wako wana kimbia badae wanakuacha baadae tuna wapa shida wakuu kwa kutojua undani kumbe umesakiziwa na wapenda vilivyo andaliwa ayaa wadau mwanetu mboso uyoooo umangani ila tarehe 9 atakuwepo Wasafi Festival19 Dar.”

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 2, 2019
Prof. Kilangi awataka wanasheria wa serikali kubadilika ''Jamii itawabadilisha''