Mkali wa miondoko ya Hip hop Farid Kubanda maarufu kama Fid Q amesema baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ataachia ngoma mpya.

Akiongea na Dar24 Media Fid Q ambaye ni mmoja kati ya wasanii watakaofanya tamasha la ‘Sports & Music Festival 2018’ litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza siku ya Eid Pili mwezi huu ameongeza kuwa mashabiki watakao hudhuria katika tamasha hilo watapata bahati ya kuwa wa kwanza kuskia ngoma zake mpya.

Tazama video ya mahojiano ya Fid Q hapa chini;

Jean-Michael Seri kucheza England msimu ujao?
Kamati yaundwa kuchunguza mwanamke aliyejifungua mikononi mwa polisi

Comments

comments